THANK YOU PBZ LTD!

TUNAKUSHUKURUNI PBZ LTD!

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) inapoazimisha miaka 52, Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi Canada, ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association), inaishukuru benki yetu hii kwa kutuondoshea Wana-Diaspora wote wa Tanzania shida iliokuwa sugu huko nyuma kwa miaka mingi ya kupeleka pesa nyumbani Tanzania (remittances) kutoka ughaibuni. 

Huko nyuma  upelekaji wa pesa nyumbani Tanzania ulikuwa mgumu sana na wengi tukishindwa kutokana na fees za juu ambazo makampuni ya multi-national conglomerates za remittances zilikuwa zikitutoza, mpaka pale Benki ya Watu wa Zanzibar ilipoingilia kati kutatua suala hili na kutuletea njia yenye bei nafuu  kwa kushirikiana na WorldRemit.

Leo tunashukuru kwani sio bei ni nafuu tu, lakini tunaweza pia kupeleka pesa nyumbani Tanzania from the palms of our hands, bila ya kuenda benki kupanga foleni na kwahivyo tunasema… THANK YOU PBZ LTD! 

Zaidi, kwa msaada huu Watanzania wote tunaoishi nje wenye kupeleka pesa nyumbani tunaipa hongera benki ya Watu wa Zanzibar kwa kusherehekea miaka 52 ya kuwahudumia wananchi na tunaitakia maendeleo makubwa zaidi mwaka hadi mwaka. 

 

“The People’s Bank, The People’s Choice in the Diaspora!”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *