WANA-ZACADIA TUNAFURAHIA UZALENDO WA PBZ LTD!

WANA-ZACADIA TUNAFURAHIA UZALENDO WA PBZ LTD!

Kitendo cha kutoa ahadi kilichofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd. (PBZ Ltd) Ndg. Juma Ameir Hafidh kwa wanafunzi wa Kidatu cha Sita wa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa wakifanya vizuri na kupata Alama ya ‘A‘ atainunua kila moja ya Alama hio kwa Shilingi Milioni Moja, kimetufurahisha sote Wanajumuia wa Zacadia ya hapa Canada.

Ahadi hiyo ambayo Mkurugenzi huyo aliitoa wakati wa hafla ya kukabidhiwa Komputa Wanafunzi 96 wa Skuli 17 za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Kisonge hivi majuzi, tunaiona ni nia safi yenye upendo ndani yake katika kuboresha elimu ndani ya Visiwa vyetu na kwahivyo hatunabudi kuipigia saluti Benki yetu ya Watu wa Zanzibar kwa kuwa mstari wa mbele katika jitihada za kuinuwa kiwango cha elimu nchini sio kwa maneno matupu bali kwa vitendo.

Tungelipendelea na mashirika mengine ya serikali na yasiokuwa ya serikali nchini kuiga mfano huu wa uzalendo wa Benki yetu ya Watu wa Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *