ZACADIA YAPOKEA RASMI SERA YA DIASPORA YA ZANZIBAR!

THE DIASPORA POLICY OF ZANZIBAR

Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi Canada iitwayo ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) jana ilipokea rasmi kitabu cha Sera ya Diaspora ya Zanzibar (The Diaspora Policy of Zanzibar) ambacho Jumuiya ilipewa copy yake hio kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein siku ya Kongamano la tano la Diaspora Tanzania lililofanyika Tibirinzi, Chake Chake, Pemba, kwenye tarehe 18-19 Agosti, 2018.

Akikiwakilisha kitabu hicho mbele ya Kamati Maalum ya Zacadia iliyokutana jana jijini Toronto, Bi Arafa Ibrahim Mustafa ambae ni Board Member wa Zacadia na ambae alihudhuria Kongamano hilo kwa niaba ya Zacadia, alisema kuwa pamoja na kukiwakilisha kitabu hicho pia anawakilisha salaam maalum kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alizozitoa kwenye Kongamano hilo akiwataka Wana-Diaspora kutambua kuwa wana jukumu lililosawa la kuijenga Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa nafasi na uwezo walionao, ikiwa kwa kiuchumi au kielimu.

Akitoa briefing ya Kongamano hilo mkutanoni jana, Bi Arafa alisema kuwa Rais Shein alisisitiza kuwa maendeleo ya kweli hayaji kwa kutupiana lawama au kwa misingi ya utashi, bali maendeleo ya kweli yanahitaji bidii na maarifa katika utetekelezaji wa majukumu, umoja na mshikamano pamoja na matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo nchini.

Sambamba na hayo, Bi Arafa aliripoti mkutanoni kuwa Rais Dk. Shein aliwahakikishia Wanadiaspora kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawakaribisha kuenda kuekeza Zanzibar na kuwahakikishia kuwa suala la ardhi wasiwe na wasi wasi nalo kwani Waziri anaeshughulika na Ardhi pamoja na Mkurugenzi wa ZIPA walikuwepo kwenye Kongamano.

Bi Arafa pia alielezeea kuwa Dk. Shein aliwasihi Wanadiaspora kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi wanazoishi na kuendelea kuwa mfano wa tabia njema ili kuendeleza sifa ya ukarimu, upendo, urafiki na usalama ambayo raia wa Tanzania wamejijengea tokea enzi na enzi na inatambulika katika mataifa yote duniani.

Pamoja na hayo bi Arafa alitamka jana mkutanoni kuwa Dr Shein aliwataka Wana-Diaspora kuendeleza kwa ari na kasi utamaduni wa kuenda kutembea nyumbani kila baada ya muda, jambo ambalo Dr Shein alisema ni muhimu na linaimarisha mapenzi. Dr Shein alisisitiza kuwa Wana-Diaspora wanapokuenda nyumbani wafanye jitihada za kuenda na watoto wao.

Kikao hichi Maalum cha Zacadia pia jana kilipokea Ripoti ya maendeleo yanayofanyika katika Kitengo cha Zacadia cha Kuhifadhi Mazingira ya nchi yetu. Kitengo hichi kinashughulika hivi sasa na kuanzisha hifadhi ya wanyama ambao wamepunguwa sana na wengine kupotea kabisa katika kisiwa cha Pemba. Hifadhi hii imo katika kuanzishwa na Zacadia katika Mkoa wa Kusini Pemba, wilaya ya Mkoani katika kijiji cha Mtangani, Mohogani. Hifadhi itakuwa  ya wale wanyama ambao kwa sasa wamepotea au ni adimu kuoneka kisiwani Pemba kutokana na sababau mbali mbali. Jina la hifadhi ni: ZACADIA WILDLIFE SANCTUARY.

Kikao pia kilipokea Ripoti ya mkutano wa kumpokea balozi mpya wa Tanzania nchini Canada (Balozi Alphayo J. Kidata) uliofanyika Ottawa wiki iliyopita. Kamati ilipendekeza kuwa Balozi aalikwe kuja kuwatembelea Watanzania wanaoishi Toronto na vitongoji vyake kwa haraka sana kabla Winter haijaanza.

SWAHILI VERSION!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *